IJUWE ZANZIBAR MPYA
ZANZIBAR MPYA NI ILE IYONGOZWAYO NA DR MWINYI
Dr Hussen Ali Hassan Mwinyi ni moja kati ya viongozi walio pambika na sifa njema na zingependwa na watu wengi duniani kote, mfano wa tabia hizo kama vile uchapa kazi, mweledi, mwenye busara na upendo kwa mananchi anao waongoza, utu, uzalendo, hata na uchangamfu unaomfanya kuongezeka kwa haiba ya tabia zake.
Ndio raisi wa awamu ya nane Zanzibar, na hajaanza kutekeleza yale aliyo waahidi wazanzibari katika viriri, kwani punde ndio kaapishwa ili kuhalalishwa kuwa raisi rasmin wa Zanzibar. Ila sio mgeni sana kwa wananchi kwani kapitia ngazi tofauti tofauti katika serikali ya mapinduzi ya zanzibar pamoja na ya muungano.
Dr. Hussen Mwinyi ameonesha jitihada za makusudi tangu hakujakucha kwani waswahili wanasema " Nyota njema huonekanwa asubuhi" ndio maana nasi hatunabudi kumshukuru mwenye-enzi-mungu kwa kutuneemesha kiongozi mahiri na jemedari kwa maendeleo ya taifa letu, kwani ameonesha namna ya kipekee ya kupitisha kampeni zake ambapo aliwashangaza wegi kwa kutembelea sehemu tofauti tofauti kwa ujasiri mkubwa ikiwemo wanafunzi wa elimu ya chini na yajuu, wakulima wakiwemo wa mwani, wafanya biashara wadogo wadogo, wajane pamoja na wavuvi ambapo ndo kajenga ngome na kunadi " UCHUMI BULUU" na kuendelea kusema kuwa yeye ni raisi wa wanyonge.
Hivyo wanzibari wanahamu na kuzisubiria neema hizo kutoka kwake haswa vijana kwani ameewahidi kwamba atatoa ajira nyingi hususan kwa vijana.
Namalizia kuandika: Karibu sana Dr Hussen Ali Hassan Mwinyi, karibu Zanzibar.
Comments
Post a Comment