FAIDA ZA TIKITIMAJI KATIKA MWILI WA BINAADAMU
JE KUNA FAIDA GANI ZINAZO PATIKANA KUPITIA TIKITIMAJI KATIKA MWILI WA BINAADAMU?
Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili na koroho bila ya kusumbuliwa na maradhi yoyote.
Duniani kuna aina nyingi za matunda, ila leo tutakwenda kuangalia umuhimu wa tunda la tikitimaji.
Tikitimaji ni moja kati ya matunda muhimu sana katika mwili wa binaadamu, kwani asilimia yake 92 limeundwa na maji pamoja na madini mbalimbali ambavyo vimebeba haiba na sifa ya pekee ya tikitimaji kama ifuatavyo:
vitami A, B6,C, nyuzinyuzi, phosphoras,madini ya chuma, protini n.k
Tikitimaji hutibu na kulainisha choo, hungarisha ngozi, huongeza kiwango cha maji mwilini, husafisha figo, huponyesha vidonda, hupunguza uzito, hupelekea mtiririko mzuri wa damu, huondosha sumu mwilini na hukinga uharibifu wa seli.
Pamoja na faida hizo, tikitimaji husaidia nguvu za kiume haswa ukila na mbegu zake, kuna L-arginine ambayo husaidia kuongeza nguvu za kiume.
pia kwa wanawake wanao jipenda na kuthamini urembo tikitimaji husaidia kuondosha madoa na weusi kwenye magoti au kisugudi, hung'arisha na kuondosha unene.

Comments
Post a Comment