Posts

ELIMU NI RASILIMALI MUHIMU KATIKA MAISHA

  ELIMU INAUMUHIMU MKUBWA KATIKA MAISHA YETU KIJAMII NA KIUCHUMI E limu ni taaluma inayomfanya mwanadamu kutoka katika ujinga na kuwa katika nuru au muamko juu ya kitu  fulani, kitaaluma, kijamii na kiutamaduni. kunausemi usemao " Elimu ni nuru" inamaana kuwa elimu ni rasilimali muhimu sana katika maisha ya mwanadamu bila ya kujali kabila, rangi, dini na hata jinsia. Katika  maandiko ya dini ya kiislamu  ina sema kuwa ni elimu ni lazima (Faradhi) kwa kila muislamu mwanamke na mwanamke. Hivyo inaonesha uzito na umuhimu wa elimu katika maisha ya kila siku, bila ya kujali aina gani ya elimu

MAENDELEO YA SEKTA YA HABARI ZANZIBAR

 YAFAHAMU MAENDELEO MAKUBWA YALIYO PATIKANWA KATIKA AWAMU YA SABA KATIKA UWONGOZI WA DR SHEIN Uandishi wa habari ni mchakato wa kuandika, kutangaza na kuchapisha habari ili kuweza kuwafikiwa hathira walio wengi katika jamii. Kuna njia tofauti tofauti ya kuwafikishia hadhira matukio na habari mbalimbali kama vile kupitia magazeti, kupitia televisheni na redio pamoja na njia ya mtandao. Dr Shein ni kiongazi mahiri sana kwani alikuwa akiongoza Zanzibar kwa weledi mkubwa, uvumilivu, ustahamilivu, akitumia busara, uzalendo, uaminifu wa hali ya juu na mtu asiye na pupa na sifa hiyo ikiongeza haiba ya ukarimu wake alio jaaliwa na muumba.  Katika awamu ya saba ya Dr Ali Muhammed Shein ni kati ya awamu iliyo ishuhulikia vyema na kuiletea maendeleo makubwa sekta ya habari kwa kuzingatia wakati wa sayansi na teknologia, Dr Shein hakuifumbia macho ZBC kwa kuiletea vifaa vya kisasa na uwongozi makini katika sekta hiyo. Mfano wa vifaa hivyo ni trasmita yenye uwezo mzuri wa kurusha matangazo...

IJUWE ZANZIBAR MPYA

ZANZIBAR MPYA NI ILE IYONGOZWAYO NA DR MWINYI  Dr Hussen Ali Hassan Mwinyi ni moja kati ya viongozi walio pambika na sifa njema na zingependwa na watu wengi duniani kote, mfano wa tabia hizo kama vile uchapa kazi, mweledi, mwenye busara na upendo kwa mananchi anao waongoza, utu, uzalendo, hata na uchangamfu unaomfanya kuongezeka kwa haiba ya tabia zake.  Ndio raisi wa awamu ya nane Zanzibar, na hajaanza kutekeleza yale aliyo waahidi wazanzibari katika viriri, kwani punde ndio kaapishwa  ili kuhalalishwa kuwa raisi rasmin wa Zanzibar. Ila sio mgeni sana kwa wananchi kwani kapitia ngazi tofauti tofauti katika serikali ya mapinduzi ya zanzibar pamoja na ya muungano. Dr. Hussen Mwinyi ameonesha jitihada za makusudi tangu hakujakucha kwani waswahili wanasema " Nyota njema huonekanwa asubuhi" ndio maana nasi hatunabudi kumshukuru mwenye-enzi-mungu kwa kutuneemesha kiongozi mahiri na jemedari kwa maendeleo ya taifa letu, kwani ameonesha namna ya kipekee ya kupitisha kampeni zake...

MADHARA YA RUSHWA KATIKA JAMII

Image
  RUSHWA NI ADUI WA HAKI. JE UNAYAJUA MADHARA YA RUSHWA KATIKA JAMII NA SERIKALI KWA UJUMLA. Rushuwa ni fedha au kitu chochote cha thamani anachopewa mtu mwenye madaraka ya jambo fulani ili mtoaji apatiwe upendeleo. Rushwa kiserikali ni usaliti kwa umma, kwasababu rasilimali za umma zinaweza kutumiwa vibaya kwa lengo la kumnufaisha mtoaji rushwa na mpokeaji.                         MADHARA YA RUSHWA Huzuia ukuaji wa uchumi. Huhatarisha utawala bora na haki za binaadamu, mfano kununua kuara wakati wa uchaguzi na kutishia mchakato wa kidemocrasia. Hupelekea kutoa nafasi za upendeleo chini ya huduma mfano huduma za afya,elimu, upatikanaji wa maji ya kunywa na makaazi. Serikali ni mdau mkuu katika kupambana na vitendo vya rushwa na kuhakikisha taasisi zote za binafsi  na serikali zianatokomeza adui rushwa. Mnamo septemba 2016serikali ilianzisha mahakama kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi ili kushuhulikia kesi kubwa...

FAIDA ZA TIKITIMAJI KATIKA MWILI WA BINAADAMU

Image
JE KUNA FAIDA GANI ZINAZO PATIKANA KUPITIA TIKITIMAJI KATIKA MWILI WA BINAADAMU? Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili na koroho bila ya kusumbuliwa na maradhi yoyote. Duniani kuna aina nyingi za matunda, ila leo tutakwenda kuangalia umuhimu wa tunda la tikitimaji. Tikitimaji ni moja kati ya matunda muhimu sana katika mwili wa binaadamu, kwani asilimia yake 92 limeundwa na maji pamoja na madini mbalimbali ambavyo vimebeba haiba na sifa ya pekee ya tikitimaji kama ifuatavyo: vitami A, B6,C, nyuzinyuzi, phosphoras,madini ya chuma, protini n.k Tikitimaji hutibu na kulainisha choo, hungarisha ngozi, huongeza kiwango cha maji mwilini, husafisha figo, huponyesha vidonda, hupunguza uzito, hupelekea mtiririko mzuri wa damu, huondosha sumu mwilini na hukinga uharibifu wa seli. Pamoja na faida hizo, tikitimaji husaidia nguvu za kiume haswa ukila na mbegu zake, kuna L-arginine ambayo husaidia kuongeza nguvu za kiume. pia kwa wanawake wanao jipenda na kuthamini urembo tikitimaji husaid...